Huwa hakikui.
Watoto wadogo huwa wana kliniki wanapima uzito na maendeleo mengine ya ukuaji.
Wanafanya hivyo ili kujua maendeleo ya watoto kwa sababu bila KUPIMA huwezi kujua kama kitu kinakua au hakikui.
Hii ina maana gani kwetu?
Unatakiwa kujifanyia tathmini kila siku, kila wiki na mwezi ili ujue maendeleo yako.
Kila unachofanya hakikisha unakipima, usiendelee na safari ambayo hujui hata wapi unaenda.
Unapojifanyia tathmini, unapata mwanga wa kujua kule unakokwenda.
Tunamwamini Mungu, lakini watu wengine WANAPASWA kuleta data.
Na namba huwa hazidanganyi, kila wakati tumia namba kufanya maamuzi na siyo hisia.
Hatua ya kuchukua leo; ukitaka kufanya maamuzi tumia namba kwa sababu namba zitakupa ukweli.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog