Huwezi Kumzuia Mtu Anayetaka Kujiua
Njia rahisi ya kuishi muda mrefu ni kuwa mwangalifu kwenye kila eneo la maisha yako.
Lakini, kuna watu wanachagua kujiua wao wenyewe. Unaweza kupambana kuwasaidia lakini wao hawasikii, hivyo unamwacha afe.
Iko hivi, kwenye maisha unajua kabisa kuna vitu ukifanya vinakupelekea kifo, na iko wazi kabisa lakini watu wengine hata uwaeleze vipi bado wanakimbilia kufanya yale yale yanayowapelekea kwenye kifo.
Kama kitu siyo sahihi usifanye, lakini mtu anajua siyo sahihi lakini anafanya, hivyo anakuwa amechagua kujiua yeye mwenyewe na huwezi kumzuia mtu kujiua.
Umeshajua ni wapi ukienda utakufa hivyo epuka kwenda sehemu hiyo.
Hatua ya kuchukua leo; Fanya kitu sahihi na kile ambacho siyo sahihi usifanye wala usiseme.
Usifanye yale mambo ambayo yatakuja kukupeleka kwenye kifo. Ninaposema kifo ni yale mambo ambayo yanapelekea wewe kupata anguko au hasara.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog