Juzi nilipokea zawadi kutoka kwa rafiki yangu Kocha Dr Makirita Amani, ni zawadi ya kijitabu kidogo ambacho amechambua ujumbe wa insha kutoka Garcia, ujumbe kwenda kwa Garcia yaani A message to Garcia.
Naomba ninukuu kama ilivyo kutoka kwa Elbert Hubbard.
Kama unamfanyia mtu kazi, mfanyie kazi kweli.
Kama anakulipa mshahara unaoweza kukupatia mkate na siagi mfanyie kazi.
Mwongelee vizuri, fikiria mazuri kuhusu yeye, simama upande wake na tetea taasisi yake.
Nadhani kama ningekuwa namfanyia mtu kazi, ningemfanyia kazi kweli.
Nisingemfanyia kazi kwa sehemu ya muda wake, bali kwa muda wake wote.
Ningempa huduma yangu yote, au kutokumpa kabisa.
Uaminifu kidogo ni bora kuliko akili nyingi.
Kama unataka kulalamika, kulaumu kupuuza, au kumbeza yule unayemfanyia kazi, ni bora ukajiuzulu nafasi yako.
Na pale unapokuwa umeacha kazi ya mtu, ni vema kukaa kimya.
Ninachokuomba ni pale unapokuwa sehemu ya taasisi, usiisemee vibaya.
Siyo tu kuisemea vibaya taasisi utaiumiza, bali pia utakua unajisemea wewe vibaya kwa sababu na wewe ni sehemu ya taasisi hiyo.
Na usisahau, kwenye biashara neno, “nilisahau, hali nafasi.
Hatua ya kuchukua leo; umejifunza nini kupitia ujumbe huu?
Unaondoka na nini cha kwenda kufanyia kazi?
Kumbuka, bosi na mteja wako ni watu wa kuwaheshimu sana, waone ni watu ambao wanafanya maisha yako yaende na kulipa bili mbalimbali.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog