Watu wengi wamekuwa hawayafurahii maisha yao kwa sababu wamekuwa wanaahirisha kuishi. Kwa mfano, mpaka nikiwa na nyumba au nikiwa na gari ndiyo nitaanza kuishi na kuwa na maisha ya furaha.
Wanasubiri mpaka kila kitu kiwe sawa ndiyo wafanye yale wanayotaka kufanya. Unapaswa kujua maisha hayakusubiri wewe uwe tayari, bali yanaendelea kwenda.
Hivyo wajibu wako ni kuyaishi maisha yako kwa ukamilifu wake badala ya kusubiri kila kitu kiwe kama unavyotaka wewe.
Tumia kila fursa kuyaishi maisha na kuyafurahia, maana mambo madogo madogo unayofanya ndiyo yanayojenga kumbukumbu kubwa kwenye maisha yako.
Kwa mfano, je, wewe ni mambo gani madogo madogo ambayo ulishawahi kufanya ukiwa mdogo na ukayakumbuka mpaka leo?
Kwa mfano, Robin Sharma anatushirikisha hadithi yake ya ujanani ambapo yeye na wenzake watatu walienda kupiga kambi porini. Walikuwa na maandalizi mazuri na walipofika walifanya kila kilichopaswa, kama kuwa na hema, kuwasha moto na mengine.
Lakini usiku walisikia mingurumo ya wanyama wakali, wakakimbia haraka na kwenda kujifungia kwenye gari.
Mpaka leo anakumbuka tukio hilo, ambalo ni dogo lakini limekuwa na kumbukumbu kubwa kwake.
Ishi maisha yako kwa ukamilifu wake kwa kuthamini mambo madogo madogo unayofanya kila siku, hayo ndiyo yanayojenga maisha ya furaha.
Hatua ya kuchukua leo; ni mambo gani madogo madogo ambayo ulishawahi kufanya ukiwa mdogo na unayakumbuka mpaka leo na yanakuletea furaha?
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog