Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ni Kipi Kikubwa Kinachoweza Kukushinda?

Kuna hadithi moja mwandishi Robin Sharma anasimulia katika kitabu chake cha The everyday Hero Manifesto.

Robin Sharma anatushirikisha mgonjwa aliyeandika kitabu kwa njia ya kukonyeza.

Unaweza kushangaa imewezekanaje, lakini tayari imeshawezekana na rekodi imeshawezekana.

Robin Sharma anatushirikisha hadithi ya Jean -Dominique Bauby ambaye alikuwa na maisha mazuri na ya mafanikio.

Siku moja akapatwa na kiharusi ambacho kilipelekea apooze mwili mzima, lakini akili yake ilibaki sawa.

Alikaa hospitalini kwa muda mrefu na akafundishwa jinsi ya kuwasiliana na watu wengine kwa kutumia macho.

Ni lugha ngumu kwa mtu kuelewa na kuitumia, lakini Bauby aliweza kuimudu vizuri.

Hilo lilipelekea aweze kutumia lugha hiyo ya kukonyeza kuandika kitabu kupitia usaidizi wa mtu wa kutafsiri.

Hilo linatuonyesha jinsi ambavyo ushujaa unawezekana kwa kila mmoja bila ya kujali nini ambacho mtu unapitia.

Kama mtu aliweza kuandika kitabu kwa kukonyeza macho, ni kipi kikubwa kinachoweza kukushinda wewe?

Bado unao uwezo wa kufanya makubwa kwenye maisha yako haijalishi nini unapitia.

Hatua ya kuchukua leo; umejifunza nini kupitia hadithi hii ya Bauby? Naomba unishirikishe kwa kuandika maoni yako.

Kama mtu aliweza kuandika kitabu kwa kukonyeza kipi kikubwa kinachoweza kukushinda wewe?

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Join the Conversation

1 Comment

  1. Hakuna kinachoweza kunishinda,naweza kufanya chochote kile provided bado niko hai, Asante sana mwalimu.

    Like

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: