Hakuna kitu kipya mpaka sasa,mara nyingi mambo ni yaleyale lakini kwa nini inakuwa vigumu watu kuchukua hatua au kufanikiwa kwenye jambo fulani?
Unafikiri ni kwa nini watu wanakuwa vilevile kila mara?
Ni kwa sababu watu wanakosa uwajibikaji.
Ni rahisi mwasibu aliyeajiriwa kufanya kazi vizuri alipoajiriwa ila ukija kwenye maisha yake binafsi hata mipango binafsi wala bajeti. Ni kwa nini kwenye ajira anafanya lakini binafsi hawezi kufanya? Ni kwa sababu anakosa uwajibikaji kwenye maisha yake binafsi lakini kwenye ajira kuna mtu anamwajibisha ndiyo maana anafanya hivyo.
Hata tukija katika maisha yetu ya kawaida, tunafanya kitu kwa haraka kama kuna mtu anatuwajibisha.
Ili uweze kufanikiwa kwenye maisha yako, unapaswa kuwa mwajibikaji kwenye kila unachopaswa kufanya.
Kukosa uwajibikaji kwa watu wengi ndicho kinachowafanya wasipate matokeo.
Hatua ya kuchukua leo; wajibika na maisha yako, usisubiri kuwajibishwa ndiyo ufanye.
Kuwa na kocha au mwalimu ambaye atakua anakusimamia na kukuwajibisha bila huruma.
Sisi binadamu huwa tunafanya pale anapokuwepo mtu wa kutuwajibisha. Hivyo, kama unataka kuona matokeo, kuwa mwajibikaji.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog