Usiwaongelee wengine vibaya, najua kuna watu wengine hawawezi kumaliza siku bila kuwasema WENGINE vibaya.
Midomo yao iko kama vile bata ambaye hawezi kujizuia pale anapotaka kujisaidia.
Nakusihi sana acha kusema watu vibaya, wewe siyo kiranja wa dunia ambaye unataka watu wawe kama vile unavyotaka wewe.
Ukikosa mazuri kwa mtu ya kusema, basi kaa kimya na siyo lazima kuongea.
Benjamin Franklin amewahi kunukuliwa akisema sitamwongelea mtu mwingine vibaya : “Kamwe nitasema yote mazuri ninayoyajua kuhusu wengine.”
Kauli hiyo imebeba msingi muhimu sana kwenye kuaminika ambao ni kutokuwaongelea wengine vibaya.
Ukitaka kuaminika na wengine, kamwe usiwaongelee wengine vibaya bali sema yale ambayo ni mazuri tu kutoka kwao.
Hatua ya kuchukua leo;
Sali sala hii kila siku;
sitamwongelea mtu mwingine vibaya , kamwe nitasema yote mazuri ninayoyajua kuhusu wengine.
Kwahiyo, sema mazuri unayoyajua kuhusu wengine.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog