Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ukitaka Kuoa Au Kuolewa Olewa Au Oa Mtu Huyu

Kwanza kabisa nikuambie tu kitu rafiki yangu nikupendaye,

Huwezi kubadilisha asili ya mtu hata siku moja. Kama ulioa au kuolewa ukiwa na lengo la kutaka kumbadilisha mtu awe kama unavyotaka wewe hapo umejidanganya.

Ukweli ni kwamba, ukitaka kuoa au kuolewa, oa au olewa na mtu ambaye hutaki kumbadilisha.

Matatizo mengi kwenye mahusiano huwa yanayokea pale mmoja anapotaka ambadilishe mwenza wake awe kama vile anavyotaka yeye.

Rafiki, usipambane na asili, asili huwa haishindwi bali wewe ndiyo utakayeshindwa.

Oa au olewa na mtu ambaye utaweza kuishi naye kwa namna jinsi alivyo lakini siyo kumbadilisha.

Kwa kila mtu unayekutana naye, kuna mazuri ndani yake hivyo basi, wewe husiana naye kwa yale mazuri ambayo umeyaona ndani yake na maisha yataenda lakini pale unapotaka kuwa kiranja wa mahusiano ndiyo unakuja kuchemka.

Umewakuta watu na tabia zao ambazo wamezijenga kwa miaka mingi halafu wewe unataka kumbadilisha kwa siku moja?

Kikubwa wewe ishi misingi yako ambayo itamfanya avutiwe na wewe na kubadilika mwenyewe.

Kwa mfano, kama wewe ni Mkristu Yesu Kristu hakukuvuta kwa mabavu uingie kwenye ukristu bali kwa upendo wake. Mafundisho yake ndiyo yalikuvuta wewe.
Halikadhalika kwa waislamu vivyo hivyo, Mohammed hajakuvuta kwa mabavu ila misingi yake ilikushawishi kiasi kwamba ukajiunga ili uwe mfuasi wake lakini hutaka kuingia ili umbadilishe bali uishi kile ambacho umekipenda toka kwake.

Hatua ya kuchukua leo; ukitaka kuoa au kuolewa oa au olewa na mtu ambaye hutaki kumbadilisha.
Na kama tayari vyote, basi usijisumbue kutaka kumbadilisha bali husiana naye kwa yale ambayo ni mazuri kutoka kwake.

Kwahiyo, Sina uhakika kama itakufaa lakini kama unatafuta ubaya kwa mtu huwezi kuukosa. Hivyo mpende yule uliyempenda kwa yale mazuri ambayo umeyaona ndani yake na mabaya achana nayo.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: