Wafanyabiashara wengi wanakosea kitu kimoja, wanaanza na bidhaa badala ya kuanza na soko.
Kabla hujazalisha tafuta kwanza soko la kwenda kuwauzia kile unachozalisha.
Unapaswa kutafuta kundi ambalo tayari lina njaa, kisha unaliuzia kundi hilo chakula.
Kwa kuwa watu wengi wanakosea kwa kuanza na bidhaa kisha kutafuta soko,wewe anza na soko kisha bidhaa.
Ukishakuwa na watu wenye uhitaji, hutakosa kitu cha kuwauzia. Lakini ukianza na bidhaa, utatumia nguvu kubwa sana kupata soko.
Hatua ya kuchukua leo; kama unataka kufanya biashara, anzia sokoni kwanza, angalia uhitaji ambao watu tayari wanao kisha njoo na suluhisho.
Kwa kufanya hivyo, kazi itakua rahisi kwako kuliko ukianza na suluhisho halafu uanze kutafuta wanaohitaji.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog