Kwenye mauzo, usihangaike sana kutaja sifa za bidhaa zako, jitahidi sana kuuza manufaa ambayo mteja atapata baada ya kununua bidhaa yako.
Huwa tunafanya makosa sana kwenye mauzo, unamwambia mteja sifa za bidhaa zako ambazo kiuhalisia sifa hazimsaidii mteja kwa changamoto alizonazo.
Mteja atafarijika pale bidhaa yako itakapokwenda kumtatulia changamoto zake. Pale bidhaa itakapokuwa suluhisho la maisha yake.
Unapokuwa muuzaji bora kuwahi kutokea, hakikisha unapokuwa na mteja mshawishi kununua kile unachouza kwa sababu kuu mbili, bidhaa unayomuuzia itakwenda kumpunguzia gharama au kumuongezea faida.
Kwa mfano, kitabu hiki kitakwenda kukusaidia kuongeza kipato chako mara mbili au kitabu hiki kitakwenda kukusaidia kuokoa gharama.
Hatua ya kuchukua leo; usiuze sifa, bali uza matokeo au manufaa ambayo mtu atayapata.
Kumbuka watu wananunua kwa sababu zao binafsi na siyo wananunua kwa sababu ya kukuonea huruma wewe. Jitahidi kutoa thamani kubwa ambayo itamshawishi mteja kununua kile unachouza.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog