Kuna wakati utajiona kama vile una kisirani, huna bahati kwa sababu kila unavyopambana kuuza huuzi.
Kuna kosa moja ambalo unafanya na kosa hilo ni kukosa shauku.
Shauku ndiyo sifa namba moja inayolipa duniani. Yeyote anayeongea kwa shauku au kufanya kitu chochote kwa shauku anakuwa anauza kile anachofanya.
Shauku ni ile hali ya uungu ndani yako, yaani unakuwa na mzuka kiasi kwamba wale wanaopokea kile unachotoa wanahamasika kukipokea pia.
Kwa mfano, wauzaji wawili wameenda sehemu kuuza, mmoja anaenda kinyonge, anauza kama hajiamini kile anachouza na mwingine ana shauku, ana tabasamu, kiasi kwamba lile tabasamu lake, lina washawishi watu kukubaliana naye.
Chochote unachofanya weka ushawishi mkubwa. Onesha shauku kubwa kwenye kila kitu, hata kama ni mtu ambaye siyo mchangamfu jitahidi kuchangamka na kuwa na shauku kwani shauku ndiyo sifa inayolipa duniani.
Unapokuwa na shauku, unawaambukiza hata wengine.
Hatua ya kuchukua leo; unavyoenda kwa mteja au mteja anavyokuja kwenye eneo lako la biashara igiza kuwa na shaku kubwa na utawafanya wateja washawishike na kukubaliana na wewe.
Yaani leo, wewe nenda kaigize shauku kwa chochote kile utakachofanya. Ukiongea na mtu na simu kuwa na shauku, tabasamu .
Kuwa na shauku ni kuamini kwenye kitu unachouza na unapokuwa huna shauku unawafanya watu wasikuamini kwenye kile unachouza hata kama unauza bidhaa bora kiasi gani.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog