Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kama Unataka Matokeo, Fanya Kitu Hiki

Rafiki yangu nikupendaye,

Kinachokukwamisha na kushindwa kupata matokeo unayotaka ni kwa sababu moja tu nayo ni sababu unazojipa.

Kuna sababu nzuri unazojipa ambazo zinakufanya usichukue hatua.

Pale unapokutana na changamoto mbalimbali unajipa sababu ambazo ambazo unaona ni za kweli na zinakufariji.

Nikuambie kitu, sababu unazojipa hazitokusaidia kulipa bili wala kubadilisha maisha yako.

Na kitakachokusaidia kupata kile unachotaka ni wewe kukaa kwenye mchakato sahihi na kufanya kile unachopaswa kufanya.

Kama hufanyi kile unachopaswa kufanya huwezi kupata matokeo unayotaka kuyaona kwenye maisha yako.

Shabaha yangu kubwa leo ni kukusihi wewe rafiki yangu nikupendaye ufanyie kazi kile unachotaka kwenye maisha yako. Usiishie kutamani tu, bali weka kazi.

Usikubali kushindwa kirahisi, pambana mpaka upate kile unachotaka. Ukiwa na nia ya dhati na ya kweli dunia inakusaidia kupata kile unachotaka.

Hatua ya kuchukua leo; kama unataka matokeo, fanyia kazi kile unachotaka kukiona.

Usiishie tu kutamani na kuwa na ndoto kubwa. Tamaa ya kupata kitu fulani ikupe hamasa ya kuchukua hatua. Kila siku jisukume kupata kile unachotaka na unapokuwa kwenye mchakato sahihi usiwe na wasiwasi utapata matokeo mazuri ni suala la muda.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: