Moja ya sababu zinazopelekea wengi kukosa furaha ni kufanya vitu ambavyo wanajua siyo sahihi.
Kitu kingine ni watu kufanya kitu huku wakitegemea matokeo fulani yatokee.
Kwa mfano, unachukua hatua, ukitegemea matokeo fulani ili uwe na furaha.
Hii ni njia ya kujitengenezea kushindwa na kujinyima furaha.
Cicero anasema furaha siyo kitu unachokipata kutokana na kupata vitu fulani kama wengi wanavyofikiri.
Bali furaha ni matokeo ya maisha unayoishi na namna unavyofanya mambo yako.
Fanya kitu lakini usitegemee kupata matokeo fulani kwa sababu matokeo yako nje ya uwezo wako hivyo unachotakiwa kufanya ni wewe kukaa kwenye mchakato sahihi na matokeo yatakuja yenyewe.
Hakuna mtu ambaye anaweza kudhibiti matokeo lakini tunaweza kudhibiti mchakato wake.
Hatua ya kuchukua leo; Fanya kilicho sahihi lakini usitegemee chochote kile.
Mtu mwenye hekima hafanyi chochote atakachoweza kujutia, hafanyi chochote kinyume na matakwa bali anafanya kila kitu kwa heshima, msimamo, umakini na usahihi. Hategemei chochote kitatokea kwa yeye kufanya, lakini pia hashangazwi na chochote kinachotokea na anarejea kila kitu kwa maamuzi yake mwenyewe na kusimamia maamuzi hayo.
Mara zote fanya kilicho sahihi, kuwa na msimamo na fanya kwa umakini utapata matokeo mazuri.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog