Design a site like this with WordPress.com
Get started

Uko Bize Siku Nzima, Umekamilisha Nini?

Kama huna kitu ambacho unajipima nacho kamwe huwezi kujua kama unaenda mbele au unarudi nyuma.

Unaweza ukajikuta bize siku nzima au maisha yako yote lakini ukija kuangalia matokeo hakuna kitu.

Changamoto kubwa ya watu kuwa bize ni kwa sababu hawana orodha ya mambo ya kufanya.

Unachotakiwa kufanya, kila siku unapoamka kabla hujaanza siku yako weka kabisa orodha ya mambo ya kufanya ndani ya siku hiyo yaani to do list.

Na orodha ya mambo ya kufanya yasizidi sita, hapa andika yale mambo muhimu ambayo unakwenda kufanya na siyo yale ambayo hayana msingi, kwa mfano unaandika nikiamka nitaenda chooni, nitapiga mswaki, unachotakiwa kuandika kazi au vitu ambavyo unakwenda kuvikamilisha.

Ukishakuwa na orodha ya mambo ya kufanya, komaa na orodha yako na acha mengine yakupite.

Pia, kwenye orodha yako anza na yale majukumu makubwa na yale madogo yaweke mwishoni kabisa.

Kama hujakamilisha to Do List Yako, yakamilishe siku inayofuata.

Kwa kuwa na orodha ya mambo ya kufanya ninakuhakikishia utapata matokeo mazuri na yenye ufanisi kuliko kuhangaika na kila kitu.

Hatua ya kuchukua leo; kuwa na orodha ya mambo ya kufanya kwenye siku yako.

Usikubali kuendeshwa na matukio, pangilia siku yako vizuri na usipoipangilia siku yako matukio yasiyokuwa na ulazima yatavuruga utulivu wako.

Kuwa na utamaduni wa kuweka mipango yako kwenye maandishi na utafanikiwa sana kuitekeleza kuliko kufanya yote kwa kichwa ndiyo maana unakuta unasahau vitu vingine.

Usiwe bize siku nzima halafu huna ulichokamilisha.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: