Ni kuwa mkweli kwanza kwako mwenyewe.
Kitu kikubwa kinachokuzuia usifanikiwe ni kujidanganya.
Wewe mwenyewe unajua wazi kabisa unapaswa kufanya nini lakini unajidanganya kwa sababu nzuri.
Katika maisha watu huwa wana sababu nzuri za kufanya kitu na sababu za kweli. Sababu nzuri ni zile za kujifariji kwa mfano, mtu anasema sijafanya kitu fulani kwa sababu nilikuwa nimechoka n.k. Ni sababu za kujitetea na kuonesha kwamba ulichofanya ni sahihi hata kama siyo sahihi.
Kwenye maisha hupaswi kujidanganya, kuwa na ustaarabu wa hali juu. Kwamba usipofanya kitu basi ni kwa sababu ya uzembe na uvivu.
Unapokuwa unajidanganya kwa njia ya uwongo huwezi kufika mbali.
Ili ufikie mafanikio makubwa, jiambie ukweli. Na ukweli utakusaidia. Achana na maisha ya ujanja ujanja kwani unapoteza muda na yanaumiza sana.
Hatua ya kuchukua leo; Jua jambo sahihi ni lipi na fanya.
Kitu cha mwisho, kuwa mkweli kwanza kwako mwenyewe na usidanganye. Pale unapokuwa unaona mambo hayaendi eneo fulani kaa chini jifanyie tathmini na ona kabisa wapi unakosea na kisha jiambie ukweli na chukua hatua mara moja.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog