Matapeli ni watu wazuri sana kwenye mauzo.
Wanapotuma meseji kila siku kwa watu elfu moja wanajua wazi kabisa hawawezi kukosa wateja ambao wanaenda kutuma hela na wakafanikiwa kuwapata.
Ndiyo maana watu wakipata ujumbe wa matapeli kwenye simu zao wengine huwa waingia laini, wananaswa. Kwa sababu gani? Wanajua ni kanuni ya asili kwamba, katika watu wengi huwezi kukosa wale ambao hawako makini.
Nimekupa mfano huu siyo kwamba mimi napendelea matapeli bali nimependa tutumie hii mbinu kwenye biashara zetu.
Kila siku watumie wateja wako ujumbe kuhusiana na biashara yako na katika hao unaowasiliana nao wako ambao watashawishika kununua kile unachouza.
Kila siku wapigie wateja wako simu. Kiwango kizuri cha kuanzia cha kupiga simu ni watu wasiopungua 10. Katika watu kumi ambao unawapigia kila siku huwezi kukosa mteja mmoja anayekuja kununua.
Kuliko kuhangaika na mitandao ya kijamii ambayo haikuingizii fedha mfukoni unaonaje ukatumia muda huo kuwapigia simu wateja wako na kuwatumia ujumbe?
Weka nguvu na akili yako yote kwenye kile unachofanya na utapata matokeo mazuri.
Na kwenye biashara, mauzo ni mchakato. Kuwa na zoezi endelevu la kuwapigia simu wateja, kuwatumia ujumbe na hata kuwatembelea wateja.
Kupiga simu na kutuma ujumbe ni vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wako hivyo unaweza kuvifanya kila siku.
Hatua ya kuchukua leo; kuwa na zoezi endelevu la kupiga simu na kutuma ujumbe kwa wateja wako kila siku.
Habari njema ni kwamba katika wateja unaowafuatilia wako ambao watakuja kununua kwako hivyo basi endelea kuweka juhudi zaidi.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog