Wateja wako wanapokaa na wewe kwa muda mrefu ndivyo unavyonufaika zaidi.
Ili ukae na mteja muda mrefu unatakiwa uendelee kumfuatilia mpaka pale atakapokufa. Na hata pale atakapokufa bado unaweza kuwafuatilia wale watu wake wa karibu na kuwafanya kuwa wateja wako.
Unahitaji kuweka juhudi kuhakikisha wateja wanabaki na wewe muda mrefu.
Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili wateja wakae na wewe kwa muda mrefu.
- Toa huduma bora sana kwa wateja wako, ambazo hawawezi kuzipata sehemu nyingine yoyote ila kwako tu. 2. Kutengeneza mahusiano mazuri na wateja wako, wafanye wateja kuwa rafiki kwako na kwa biashara yako, waone siyo tu wanakuja kununua, bali wanakuja kwa rafiki yao, anayewajali na kuwapa kile kilicho sahihi kwao. 3. Weka mbele maslahi ya wateja wako na siyo faida unayotaka kupata.
4. Waelimishe wateja wako, washauri vizuri, hata kama utapoteza mauzo, lakini hilo litawajengea imani zaidi na hivyo kuendelea kununua zaidi.
5. Wafanye wateja wako kuwa mashabiki wa biashara yako.
Hatua ya kuchukua leo; tumia njia hizi tano ulizojifunza hapa ili kuongeza thamani kwa wateja wako hatimaye wakae na wewe muda mrefu.
Jitahidi kutumia kila unachojua ili kuongeza mauzo. Ustaarabu pekee kwenye biashara ni kuuza, weka nguvu kubwa sana kwenye mauzo na jenga biashara yako pia.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog