Design a site like this with WordPress.com
Get started

Acha Ujuaji

Watu wengi wanajikuta wao ni wajuaji lakini bado wanafanya ujinga.

Ujinga ni kufanya kitu kile kile kwa mtindo ule ule halafu unategemea kupata matokeo tofauti.

Watu wanajikuta wao ni wajuaji kwenye biashara, mahusiano, kazi na kadhalika. Wanajikuta wajuaji lakini bado hawana matokeo mazuri.

Ujuaji una wamaliza watu wengi kwa kutokujisumbua kujifunza.

Watu tayari wanajiona wanajua kila kitu, hawataki kujifunza na kuwa wanyenyekevu wa kujifunza ndiyo maana maisha yanawapiga pia.

Kwenye haya maisha, hekima pekee unayopaswa kuwa nayo ni kujua hujui kitu.

Ukikaribisha kiburi, utaanguka kirahisi sana.

Acha kung’ang’ania mitazamo au falsafa ulizonazo ambazo hazikusaidii kusonga mbele.

Kama watu wanafanya na wanafanikiwa iweje wewe hutaki kubadilika?

Hatua ya kuchukua leo; Kuwa tayari kujifunza na kubadilika.

Acha ujuaji ambao unakaribisha anguko kwenye maisha yako.
Kaa kwenye mchakato na utakutana na bahati yako.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: