Kama unataka bahati kwenye maisha yako, amini kwenye mchakato sahihi.
Utapata matokeo pale utakapokaa kwenye mchakato.
Unaweza kujiona una nuksi lakini ukweli ni kwamba wewe huna nuksi, tatizo lako ni kwamba hutaki kukaa kwenye mchakato sahihi ili ukutane na bahati yako.
Bahati zipo, ila bahati inataka ikukute ukiwa unafanya kitu yaani ukiwa umekaa kwenye mchakato.
Haijalishi kwa sasa unapitia nini au unapata matokeo gani, kikubwa ninachokusihi kufanya ni wewe kuendelea kuamini kukaa katika mchakato.
Kila kitu kwenye maisha kinahitaji mchakato, na utapata matokeo mazuri pale tu utakapokuwa umekaa kwenye mchakato sahihi.
Hatua ya kuchukua leo; Kama unataka kukutana na bahati yako, basi amini kwenye mchakato sahihi.
Kumbuka, bahati ni pale fursa inapokutana na maandalizi.
Na maandalizi yako ni kuendelea kukaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachopaswa kufanya.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog