Design a site like this with WordPress.com
Get started

Watu Wengi Huwa Hawafanyi Hivi

Watu wengi wanapopitia changamoto au kufikia katika hali fulani ya mkwamo huwa wanafanya kosa moja ambalo ni kushindwa kukaa chini na kujitafakari.

Huwezi kujua kujua kama wapi umekosea au wapi umepatia kama hutengi muda wa kujitafakari.

Kama unapitia hali yoyote ambayo siyo ya kawaida kwako, hakikisha unapata muda wa kujisikiliza wewe mwenyewe.

Katika hali hiyo unayopitia wewe unaweza kufanya nini ili kuathiri hali hiyo uliyopata.

Wakati mwingine unajiuliza je, na wewe umechangiaje kutokea kwa kile kilichotokea?

Bila kujihoji, huwezi kupata mabadiliko ya kweli. Huwa tunakua na changamoto mbalimbali lakini huwa hatukai chini na kujiuliza namna ya kutoka kwenye hiyo changamoto.

Wewe unayo majibu ya kila aina, akili yako inayo majibu ya kile unachopitia tatizo huishirikishi unaona kama watu wengine ndiyo wanaweza kukusaidia.

Hatua ya kuchukua leo; kwa chochote ambacho unapitia pata muda wa kujitafakari na kuona kwa jinsi gani unaweza kupata ufumbuzi.

Itumie akili yako vizuri, inayo majibu, jihoji na andika yale yote unayoweza kufanya.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: