Design a site like this with WordPress.com
Get started

Lazima Upitie Maumivu Kati Ya Haya Mawili

Maisha ni maumivu, huwezi kukwepa hata siku moja. Kila mmoja anapitia maumivu yake.

Jim anatuambia; “We must all suffer one of two things: the pain of discipline or the pain of regret.”
Akimaanisha kila mmoja wetu lazima ataumia na kimoja kati ya hivi viwili;
maumivu ya nidhamu au maumivu ya majuto.

Iko hivi, ili kupata chochote kwenye maisha yako, unahitaji nidhamu ya hali ya juu sana. Nidhamu ya kuamua na kufanya na siyo nidhamu ya kujibembeleza.

Na nidhamu, kwa maneno ya kawaida tu tuseme ni kujitesa, maana itabidi ujikatalie vitu vizuri ulivyozoea ili kupata kile unachotaka.

Sasa wengi hawapendi maumivu ya nidhamu, wanajiambia kabisa hawawezi kujitesa.

Kitu ambacho wanakuwa hawajajua ni kwamba, kwa kukataa maumivu ya nidhamu, wanajipeleka wenyewe kwenye maumivu ya majuto.

Kwamba maisha yao yote wataumia kwa majuto kwa nini hawakuchukua hatua fulani na maisha yao yangekuwa bora zaidi.

Ubaya wa maumivu ya majuto ni kwamba utaenda nayo maisha yako yote.

Hatua ya kuchukua leo;
Amua leo ni maumivu gani unayataka, ya nidhamu au ya majuto, na usijidanganye kwamba unaweza kukwepa maumivu kwenye haya maisha, hicho kitu hakipo.

Amua leo, uteseke kwa nidhamu au upate maumivu ya majuto. Wewe unachagua wapi?

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: