Mwandishi na aliyekuwa muuzaji mzuri sana wa magari Joe Girard, ambaye aliingia kwenye kitabu cha maajabu cha dunia, GUINESS, kama muuzaji bora sana kuwahi kutokea hapa duniani, anatushirikisha jinsi gani KILA MTU, ANAWEZA KUUZA CHOCHOTE KWA MTU YEYOTE kupitia kitabu chake cha jinsi ya kuuza chochote kile kwa mtu yeyote.
Kupitia mauzo tunapata zawadi mbili, moja kupata fedha na pili kupata urafiki.
Lakini, watu wengi wanaingia kwenye mauzo kwa lengo la kwanza la kuangalia kupata fedha pekee na hivyo kuwa tayari kufanya chochote ili wauze.
Tamaa ya kupata fedha huwa inapelekea watu wengi kuwapoteza wateja waliokuwa nao.
Kama utamuuzia mtu kitu ambacho hakimfai jua siyo tu utampoteza mteja huyo bali utawapoteza na wateja wengine wengi.
Unahitaji kutengeneza urafiki na kila mteja wako, kwa kujali hasa hitaji lake na kuhakikisha anarudi kununua kwako na anawaambia wengine kuhusu unachofanya.
Jali maslahi ya mteja na mpatie huduma bora kiasi kwamba itamfanya arudi tena kununua kwako.
Kama unalenga kupata fedha pekee na ukakosa urafiki na wateja wako hutadumu kwenye biashara kwa muda mrefu.
Ili udumu kwenye biashara yako, jenga urafiki wa kudumu na mteja wako na usiangalie fedha pekee kutoka kwa mteja.
Hatua ya kuchukua leo; Jenga urafiki na wateja wako. Jali maslahi yako na wao watajali maslahi yako pia.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog