Design a site like this with WordPress.com
Get started

Fanya Kazi Masaa Mengi Au Uondoke

Tajiri namba moja duniani Elon Musk hivi karibuni amenunua mtandao wa Twitter. Kwa kuwa huyu Bilionea ni mtu anayeamini kwenye kazi sana, hivyo amewataka wafanyakazi wake wafanye kazi sana.

Amewaambia wana machaguo mawili,
Moja wafanye kazi masaa mengi
Mbili au waondoke.

Hapa tunajifunza kwamba, kazi ndiye rafiki wa kweli.

Huwezi kupata mafanikio makubwa kwa kufanya kazi masaa machache, ili ufanikiwe lazima ufanye kazi masaa mengi.

Asikudanganye mtu kwa kukuambia kwamba unaweka kazi kidogo halafu akili kubwa.

Kazi lazima ifanyike, kama Bilionea namba moja duniani anasisitiza kazi wewe ni nani? Fanya kazi au ondoka.

Kama hutaki kufanya kazi, basi kufa lakini kama unataka kufanikiwa basi fanya kazi.

Kama una msaidizi ambaye anakusumbua mwambie una machagua mawili, kufanya kazi au kuondoka.

Usifanye utani kwenye kazi, fanya kazi na kazi itakulipa.

Matatizo mengi yanayotokea kwenye maisha yetu ni kwa sababu ya watu kutokufanya kazi. Mtu anayefanya kazi hawezi kukosa fedha ya kutatua matatizo yanayomsumbua.

Acha ujanja, ujanja, weka kazi na utaona matokeo.

Hatua ya kuchukua leo; Fanya kazi au kama hutaki kufanya kazi chagua kufa kwa sababu huna maana kwako mwenyewe na kwa dunia kwa ujumla.

Ng’ara pale ulipo panda, nyota yako iko kwenye kile unachofanya. Kifanye vizuri ili nyota yako na ing’are.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: