Unaweza kufikiria biashara inayofanikiwa ikoje? Hebu pata picha.
Biashara inayofanikiwa siyo ile inayokuwa bora, bali ile inayokuwa ya kwanza kwenye akili za wateja.
Je, watu wakiwa wanataka huduma unayotoa, huwa wanaifikiria biashara yako?
Kama biashara yako haiko kwenye akili za watu ni ngumu kufanikiwa.
Kwa chochote kile unachouza, hakikisha watu wanajua unauza nini, watu huwa wanafanya maamuzi kwa kitu ambacho kipo akilini mwao. Ni ngumu kuanza kutafuta kitu ambacho hajakisikia kwenye masikio yake.
Itangaze biashara yako, ifanyie masoko, acha watu wajue kuhusu biashara yako.
Hatua ya kuchukua leo; ifanye biashara yako kuwa kitu cha kwanza na mteja aifikirie biashara yako pale anapokuwa anataka huduma au bidhaa unayouza wewe.
Hakikisha biashara inakuwa kwenye akili za wateja ndiyo itakuwa njia rahisi ya wewe kuuza.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog