Iko hivi rafiki yangu nikupendaye,
Kwa chochote kile unachotaka kwenye maisha yako, utakipata kwa watu wengine.
Mafanikio unayotaka kuyaona kwenye maisha yako, watakaokusaidia kupata ni watu wengine.
Kifupi kile tunachotaka tutakipata kupitia watu wengine, watu wanakutegemea ili wafanikiwe kupitia wewe.
Unahitaji kuwa na mtandao wa watu ambao wanaweza kukusaidia kwenye maeneo mbalimbali na wewe pia unaweza kuwasaidia.
Hatua ya kuchukua leo; Imarisha muungano na mahusiano yako na wengine.
Kuwa na mahusiano mazuri na watu, kwa sababu watu ndiyo kila kitu kwenye maisha yako.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog