Design a site like this with WordPress.com
Get started

Fanya Kitu Hiki Muhimu Kwako

Fanya kile ambacho ni muhimu kwako na siyo ambacho ni rahisi kwako.

Kwa sababu, kila mtu anataka kukata kona, kila mtu anatafuta njia ya mkato ya mafanikio.

Kila mtu anatafuta njia ya kupata fedha bila ya kufanya kazi.

Usiwe katika watu hao, wewe fanya kazi halali na upate fedha halali.

Usitafute kilicho rahisi, kwa sababu mwisho wa siku maisha siyo fedha tu.

Unaweza kuzipata fedha kweli na bado ukaona maisha hayafai.

Hatua ya kuchukua leo; fanya kitu sahihi na epuka njia za mkato.

Kwa chochote unachokifanya, kifanye kwa uaminifu mkubwa.
Kuwa na nidhamu, uadilifu na kujituma kwenye kila eneo la maisha yako.

Msingi wetu wa mafanikio

utii, ubunifu na kujituma.

Falsafa yetu ni;

Upendo.
👉Nitaanza kujipenda mimi  mwenyewe kwanza.
Kisha nitawapenda wengine na
Nitapenda kile nachofanya.

👉Msingi wa falsafa ya ustoa
Nitapambana na kile kilicho ndani ya uwezo wangu. Kile ambacho kipo nje ya wangu  nitaachana nacho au  kukabiliana nacho.

👉Kitu kama siyo sahihi sitafanya, kitu kama siyo kweli sitosema.

Ukawe Na Siku Bora Sana
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504

https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: