Kitu cha kwanza kinachowasukuma watu kununua ni haiba ya muuzaji. Na haiba ya mtu inatokana na tabia ambazo mtu anazo.
Ili kufanikiwa kwenye jambo lolote, unahitaji kuwa na tabia nzuri ambazo zinawafanya watu kukubaliana na wewe.
Kumbuka ndege wanaofanana huruka pamoja, hivyo kuwavutia watu wa aina fulani, lazima uwe kama wao.
Hatua ya kuchukua leo; kuwa na haiba na tabia nzuri zitakazokuwezesha kukubaliana na wengine.
Hivyo basi, mauzo ni maonesho. Mwonekano wako una mchango mkubwa sana kwenye mauzo, hivyo wauzaji wenye mwonekano wa kuvutia wanauza zaidi kuliko wengine wasio na mwonekano wa kuvutia.
Mwonekano, uongeaji, kujiamini kote kunachangia kumshawishi mtu kununua au kutokununua kwa anayemuuzia.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog