Design a site like this with WordPress.com
Get started

Unakuwa Wa Maana Pale Unapofanya Hiki

Rafiki yangu nikupendaye,

Kwenye maisha unakuwa wa maana pale unapotimiza wajibu wako.

Kwenye biashara unakuwa wa maana pale unapotekeleza wajibu wako kwenye biashara. Na ustaarabu wa kwanza kwenye biashara ni kuuza na kama huuzi kwenye biashara basi unapoteza maana.

Unapoteza maana kama uko kwenye kazi fulani halafu huifanyii kazi hiyo kazi.

Unapoteza maana kwenye mahusiano ya ndoa kama uko kwenye ndoa lakini unaishi kinyume na maadili lakini pia kinyume na misingi ya ndoa. Ustaarabu pekee kwenye ndoa ni uaminifu ukiwa mwaminifu utafanya ndoa yako kuwa na maana.

Ukiwa eneo lolote lile na hutimizi wajibu wako hiyo ni dhambi na siyo tu dhambi bali unakuwa kero kwa wengine.

Chochote kile ambacho unafanya kinyume na utaratibu huwa asili inakuadhibu. Asili haimpendelei mtu yeyote yule ambaye anakwenda kinyume na asili.

Hatua ya kuchukua leo; Jua wajibu wako ni nini na timiza wajibu na kinyume na hapo unakuwa huna maana.

Maana yako inaonekana pale tu unapotimiza wajibu wako. Kama uko hapa duniani kwa ajili ya kazi fulani basi fanya hivyo ili ilete matokeo mazuri kwa watu na siyo vinginevyo.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: