Dunia itakuwa sehemu salama kwa kila mmoja wetu endapo kila mmoja wetu atatimiza wajibu wake.
Matatizo mengi yanayotokea ni watu kushindwa kutimiza majukumu ipasavyo.
Ukishindwa kutimiza wajibu wako jua kwamba unawaumiza wengine.
Kila mmoja wetu anamtegemea mtu mwingine ili maisha yake yaende. Endapo unasitisha kile unachofanya basi unakuwa siyo tu kufanya dhambi lakini unaifanya dunia kuwa siyo sehemu salama kuishi.
Nafasi uliyopata itumie vizuri sana, acha uvivu na uzembe kumbuka unafanya kazi yako vizuri unakuwa unawasaidia wengine pia.
Kwenye kitabu cha Biblia kinasema, tafuteni kwanza ufalme wa Mungu. Na ufalme wa Mungu ni kuwatumikia watu wake.
Kwa mfano, ukiweza kumsaidia mtu kwenye changamoto yake na akapona hapo unakuwa umefanya kazi ya Mungu na umetafuta ufalme wake.
Kupitia kazi, biashara, huduma au kile tunachofanya ndipo mali nyota zetu zipo na utakatifu wako utapatikana hapo.
Hatua ya kuchukua leo; Je, unajua wajibu wako? Nenda kautimize leo kwa ukamilifu na fanya kwa moyo kwa sababu ni wajibu wako kufanya.
Kitu cha mwisho, kwa chochote kile unachofanya jua kuna watu wanakutegemea hivyo unapokuwa hufanyi unakuwa unawaangusha wengine lakini pia unawaumiza.
Fanya kazi yako ili dunia iweze kuendelea kuwa bora na sehemu salama ya kuishi kwa kila mmoja wetu.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog