Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mbinu Nzuri Ya Kutumia Pale Unapoona Umetingwa Na Mambo Mengi

Ukiona umebanwa na una mambo mengi ya kufanya huku muda wako ukiwa mchache unapaswa kufanya yafuatayo;

Moja, futa yale yote yasiyo na tija kwako. Watu wengi wanasema wako bize lakini kwenye mambo ambayo hayana tija kwao. Jiulize, hicho kinachokufanya uwe bize kinaleta fedha mfukoni?

Kama jibu ni ndiyo, endelea kukifanya lakini kama jibu ni hapana, acha mara moja.

Mbili, fokasi kwenye vipaumbele vyako. Baada ya kufuta visivyokuwa na maana, wewe akili yako yote ihamishie kwenye vipaumbele vyako muhimu.

Tatu, kaa kwenye mchakato sahihi wa kupambana na yale muhimu tu na kusahau kile kinachoendelea duniani.

Kifupi, mwisho wa siku hutakuja kuwaambia watu ni namna ulivyokuwa mzururaji bora kwenye mitandao ya kijamii na kuwa kinara kwenye mambo yasiyokuwa na mashiko.

Hatua ya kuchukua leo; nenda katumie muda wako vizuri kwenye mambo ambayo ni muhimu tu na kusahau mambo mengine ambayo siyo muhimu kwako.

Kumbuka, unao muda wa kufanya mambo muhimu tu lakini huna muda wa kufanya kila kitu kwenye maisha yako.
Unao muda mwingi mpaka unauchezea kwenye mambo yasiyokuwa na tija.
Kama huna muda unapataje sasa muda wa kufanya mambo yasiyokuwa na tija kwako?

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: