Pata picha unatoka nje ya nyumba yako unaona moshi unatoka mahali na ukakimbilia kuondoa moshi huo, kawaida hutazuia moshi kuendelea kutoka kwa sababu kwa akili za kawaida kabisa penye moshi, chini pana moto.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye watu, unapomwona mtu yupo kwenye matatizo, jua kuna kitu kimesababisha.
Sasa ukikimbilia kumsaidia kumsaidia mtu kuondokana na matatizo bila ya kujua kwa nini ameingia kwenye matatizo hayo, msaada wako hautakua na maana.
Hivyo basi, hatua ya kuchukua leo ni;
Kabla hujamsaidia mtu, jua kwanza nini kimemuingiza kwenye matatizo aliyonayo.
Usinunue matatizo ya watu, jua kwanza chanzo chao kisha ndiyo uwasaidie usijikute unazima moshi wakati moto bado uko chini.
Na usikubali yale maelezo ambayo watu wanakupa, kwamba hawana hatia, kwamba hakuna chochote kibaya wamefanya. Kila tatizo ambalo mtu anapItia, kuna namna amelisababisha au amelichochea.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog