Rafiki yangu nikupendaye,
Pamoja na madhaifu yako, bado wewe ni muhimu.
Moja ya mambo yanayopelekea tusijijali sana ni kwa sababu tunajijua sisi wenyewe kuliko mtu mwingine anavyotujua, kuliko tunavyowajua watu wengine.
Sasa inapotokea pale tunapojikumbusha madhaifu yetu, mabaya ambayo tumewahi kufanya huko nyumaz tunajiona tunastahili mateso na hivyo kutokujijali kama tunavyowajali wengine.
Tunakuwa tunajiona sisi tuna hatia na wengine hawana hatia, na ndiyo maana tunaweza kuwasaidia wengine kuliko tunavyoweza kukusaidia sisi wenyewe.
Hatua ya kuchukua leo; Jijali kama unavyowajali watu wengine na licha ya madhaifu yako jione bado una umuhimu mkubwa.
Usijichukulie poa kabisa licha ya madhaifu yako.
Tunapaswa kujikumbusha kwamba pamoja na madhaifu yetu na mabaya ambayo tumewahi kufanya bado tunastahili kujijali kama tunavyowajali wengine.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog