Design a site like this with WordPress.com
Get started

Maisha Gani Haya?

Kwako rafiki yangu,

Usikubali kuishi maisha ambayo hayana maana hapa duniani.

Usikubali kuishi bila kujifunza, unapojifunza unapata hekima ya kukuwezesha kufanya maamuzi.

Usikubali kufanya kazi pasipo kuwekeza wala kuweka akiba. Uwekezaji unakuza utajiri wako na akiba inakulinda wakati unauhitaji wa fedha.

Usikubali mtu akupite kwenye kazi, kubali watu wakupite maeneo yote lakini usikubali upitwe katika kazi na kujifunza pia.

Usikubali kila siku kuhudumia wateja wale wale kwenye biashara yako, kila siku ongeza na saka wateja wapya.

Usikubali kuishi na dhambi hizi mbili, uvivu na uzembe. Jitahidi kujituma na kuwa makini kwenye maisha yako.

Kujitegemea siyo kujitosheleza lakini pendelea kujitegemea zaidi katika mahusiano yako na wengine. Watu watakushusha thamani pale tu utakapoanza tabia ya kuombaomba hela. Jitegemee, maisha ni yako hivyo basi usiwasumbue WENGINE.

Kama unafanya biashara, jitahidi kutoa huduma bora, fanya masoko, ongeza mauzo. Jitahidi sana kufanyia kazi eneo la mauzo, maana mauzo ndiyo yanaleta fedha kwenye biashara na ndiyo uhai wa biashara ulipo.

Hatua ya kuchukua leo; fanya kile unachopaswa kufanya. Kama hufanyi kile unachopaswa hiyo ni dhambi na unawaumiza wengine.

Kama unayafurahia maisha unayoishi endelea nayo na kama huyafurahii maisha unayoishi chukua hatua mara moja. Inatosha kulalamika kwa sababu ushindi hauji kwa kulalamika chukua hatamu ya maisha yako kwa kufanya kazi.
Kila kitu kinawezekana kama kweli umejitoa kufanikiwa kwa moyo wa dhati kabisa.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: