Kiasili hakuna kitu kibaya wala kizuri. Kila kitu kipo kadiri ya mtazamo wako.
Mtazamo uliokuwa nao leo ndiyo unakufanya uwe hivyo ulivyo leo.
Una mtazamo gani juu ya utajiri, kazi, biashara, mahusiano n.k?
Ondoa dhana hii kwamba, nimeumizwa, na hakuna atakayeweza kukuumiza.
Unaumizwa kwa sababu wewe umejenga hiyo dhana kwamba umeumizwa.
Hakuna anayekuumiza, ila kinachokuumiza ni tafsiri zako mwenyewe.
Unakuta hata muda mwingine tunajenga tafsiri ambazo hata hazipo kiuhalisia na zinakuja kutuumiza baadaye.
Hatua ya kuchukua leo; usijiumize kwa sababu ya tafsiri zako binafsi.
Ondoa dhana ya kwamba umeumizwa na hakuna atayekuumiza.
Ifikie mahali ukomae na uwe na ngozi ngumu. Jifunze kupuuzia baadhi ya mambo ili maisha yako yaende. Ukiwa ni mtu wa mtazamo wa kuumizwa basi utakua unaumizwa kila wakati.
Kumbuka, hakuna kinachokuumiza zaidi ya mtazamo na tafsiri zako. Mtazamo ulionao juu ya kitu au mtu fulani ndiyo unakuletea matokeo unayopata. Unamfikiria mtu ana tabia za kishetani na mtazamo wako wote unawaza mabaya juu ya mtu huyo unafikiri utapata matokeo chanya kutoka kwake?
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog