Kiasili kila binadamu anapenda kusifiwa. Kila binadamu anapenda kuonekana anathaminiwa.
Kitu ambacho kinavuruga mahusiano yetu na wale tunaohusiana nao ni kukosoa.
Kwa mtu yeyote yule unayehusiana naye, ukitaka kuboresha mahusiano yenu, iwe ni ya kazi, biashara, ndoa na nk msifie na usimkosoe.
Wapende na wachukulie watu kama walivyo. Tafadhali kazi yako isiwe ya kukosoa bali kusifia.
Watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwenye maisha kwa sababu ya tabia ya kukosoa na siyo kusifia.
Binadamu ni viumbe vya hisia, kadiri unavyomsifia kitu cha kweli kabisa kutoka ndani yake inakuwa ni rahisi sana kujenga ushawishi mkubwa.
Watu wako tayari kukupa kile unachotaka kutoka kwao kama tu utaweza kuwa upande wao. Na watu wanakuwa huru kukupa koneksheni mbalimbali kama tu ukiwa umewasifia na siyo kuwakosoa.
Hatua ya kuchukua leo; ukitaka kufanikiwa kwenye maisha yako, wasifie watu kwa sababu watu wanapenda sifa na watakua tayari kukusaidia kukupa kile unachotaka.
Usiwe mtu unayeona mabaya tu kwa mtu. Kwa kila mtu unayekutana leo, kuna kitu kimoja cha kuweza kumsifia. Kamwe huwezi kukosa, ukikutana na mtu angalia kitu gani cha kweli ambacho unaweza kumsifia kwa namna hiyo utaweza kujenga ushawishi mkubwa na kuboresha mahusiano yako.
Vitu vya kusifia viko vingi, kwa mfano, ukikuta mtu amevaa vizuri, amevaa jezi ya timu yake msifie yale mazuri kutoka kwenye timu yake.
Sina uhakika kama itakufaa lakini ukitaka kufanikiwa sifia na ukitaka kutokufanikiwa kusoa watu.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog