Kwa sababu huna kitu kinachokusukuma kufanya.
Watu wengi wanaondoa uvivu, uzembe kama kuna kitu kinawasukuma ndani yao kufanya.
Kama huna sababu inayokusukuma ya nini kujitesa? Ila ukiwa na sababu unakuwa unajisukuma kweli na huoni tena mateso bali unaona mateso ndiyo njia ya kupata kile unachotaka kwenye maisha yako.
Mtu mmoja alikuwa na hali mbaya sana ya kiuchumi, alikuwa amekata tamaa, mauzo ya biashara yake yalikuwa kidogo lakini pia hata yeye ilifikia mahali akajiona hana anachoweza kufanya tena.
Lakini, cha ajabu mtu huyo, alipata kitu kinachomsukuma kwa nini anapaswa kuamua na kufanya kazi. Mke wake alimwambia maneno haya, mume wangu, unakata tamaa je, watoto watakula nini?
Hayo maneno yalimuumiza sana mwanaume, akamua kuamka na kufanya kazi kwa bidii, aidha apambane watoto wale au aifie akipambana.
Unaweza kuona familia uliyonayo ni kikwazo cha wewe kutofanikiwa lakini nakuambia msalaba ulionao au familia uliyopata ndiyo chanzo cha wewe kufanikiwa.
Familia yako ikupe hamasa, familia yako inakutegemea, ukishajua kwamba unategemea uvivu wote na uzembe unaweka pembeni.
Sikufichi sisi binadamu tunao uwezo mkubwa sana ndani yetu, na kwa taasisi yako mpaka sasa unatumia asilimia 10 tu ya uwezo wako. Vipi kama ukitumia hata nusu ya uwezo wako leo hii ungekuwa wapi?
Ondoka na hamasa hapa ya kwenda kufanya kazi, kumbuka familia inakutegemea rafiki yangu, usifanye kitu ambacho hakileti fedha kwenye maisha yako.
Kuwa na kitu ambacho kinakusukuma kila siku. Vuta picha una familia yako ambayo unaipenda sana na hutaki ipate shida, watoto wako wanakupenda na kukutegemea sana halafu wewe unazingua utajisikiaje?
Pata hasira za kupambana familia yako na wewe uwe na maisha mazuri. Familia yako isikie mafanikio makubwa kwa watu wengine bali kwako. Pambana, kwani inawezekana bila shaka yoyote ile.
Hatua ya kuchukua leo; Kuwa na kitu kinachosukuma kuchukua hatua na kukupa hamasa ya kuendelea na mapambano.
Rafiki yangu, pambana ufanikiwe, hakuna mtu wa kuondoa laana ya umasikini kwenye familia yako na hata dunia zaidi yako. Ukishakuwa tajiri wewe utawasaidia na wengine kuwa matajiri.
Pambana kwa sababu unajua kuna watu wanakutegemea na usipofanya hivyo unawaumiza na utajisikiaje kama unawaumiza wengine kwa sababu ya kutowajibika kwako?
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog