Tafuta mali lakini pia,
Hakikisha unayaishi maisha yako kwa ukamilifu.
Usiishi kama nyuki, ambaye anatumia maisha yake yote kutengeneza asali halafu hali yeye asali hiyo, ila inaliwa na wengine.
Watu wamekuwa wanatoa maisha yao yote kutafuta mali, ambazo hawapati hata muda wa kuzitumia na kuzifurahia, katika harakati hizo wanakufa na kuwaacha wengine wakitumia hovyo mali ambazo wamekazana kutafuta.
Pamoja na watu kukazana na kuwa na mali nyingi kwenye maisha yao, huwa hawapati utulivu wa nafsi na kuridhika na maisha yao, kwa sababu wanatumia muda mwingi kuangalia nje wana nini badala ya kuangalia ndani yao wana nini na kuimarisha kile kilichopo ndani.
Hatua ya kuchukua leo; Tafuta mali, lakini pia hakikisha unayaishi maisha yako kwa ukamilifu.
Kwahiyo, ishi maisha yako kwa kutafuta mali lakini pia pata muda wa kutumia kile unachotafuta na usiwe kama nyuki kuishi maisha yako yote kutengeneza asali halafu huli asali hiyo.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog