Design a site like this with WordPress.com
Get started

Usisubiri Mpaka Uwe Tayari

Ukisubiri mpaka kila kitu kiwe vizuri ndiyo uanze, kuna vitu unaweza kupata lakini ni vile vilivyoachwa na wale walioanza kabla ya hata ya kuwa tayari.

Kama umeiona fursa ya biashara lakini hujaanza kwa sababu hujawa tayari, utakapokuwa tayari kuanza utapata wateja lakini ni wale ambao waliachwa na wale ambao waliweza kuanza kabla hata hawajawa tayari.

Abraham Lincoln aliwahi kunukuliwa akisema, mambo yanaweza kuja kwa wale wote ambao wanasubiri, lakini watapata yale tu yaliyoachwa na wale ambao hawakusubiri mambo yawe sawa.

Hatua ya kuchukua leo; chochote unachotaka kwenye maisha yako, usisubiri mpaka uwe tayari kwa kila kitu, bali anza mara moja na utaona hatua zaidi za kupiga.

Kwahiyo, maisha siyo kusubiri bali ni kuchukua hatua kwa chochote kile unachotaka kukiona kwenye maisha yako. Ukiendelea kusubiri utakuja kupata lakini utapata mabaki yaliyoachwa na wale walioamua kuchukua hatua bila kusubiri wawe vizuri.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: