Njia bora ya kuwapenda watu na kujenga mahusiano bora ni kuwakubali watu kama walivyo. Bila ya kutaka wabadilike au wawe kama unavyotaka wewe.
Lakini, ukishaanza kusema unawapenda watu kwa sababu wako kwa aina fulani na ukishaanza kutaka watu wabadilike na kuwa kama unavyotaka wewe ndiyo uwapende, jua hapo hujawapenda watu.
Kamwe haitatokea kila mtu kwenye maisha yako kuwa kama unavyotaka wewe.
Na watu hawatabadilika kwa namna unavyotaka wewe.
Kila Mtu ana utofauti wake, ana changamoto zake pia ana mchango fulani kwenye maisha yako.
Hatua ya kuchukua leo; wapende watu na kuwakubali kama walivyo.
Jihusishe na kile ambacho unanufaika nacho kutoka kwa mtu mengine achana nayo. Pata kile unachotaka na mengine siyo shabaha yako. Ili mradi unanufaika na mtu kwenye kitu fulani, basi weka nguvu yako hapo.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog