Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kama Unataka Matokeo Tofauti

Basi panda juhudi tofauti.

Msingi mkuu unaopaswa kuujua kwenye maisha yako ni sheria ya usababishi au sheria ya kupanda na kuvuna.

Kila kinachotokea kwenye maisha yako, umekisababisha wewe mwenyewe. Yaani unachoona sasa ni mavuno ya ulichopanda huko nyuma.

Kiasili, dunia haina upendeleo. Mafanikio na furaha yako kwenye maisha inategemea misingi ya asili ya dunia.

Ukiijua na kuiishi misingi hii utakua na maisha yenye furaha na mafanikio makubwa.

Usipoijua na kuiishi, maisha yako yatakuja magumu bila ya kujali umetokea wapi na uko wapi.

Dunia haina upendeleo na mtu yeyote, wala haimpendelei yeyote, kama unaona wewe unaweka juhudi sana lakini maisha yako ni magumu, lakini kuna mtu mwingine haweki juhudi kama wewe ila maisha yake ni rahisi jua kabisa kuna misingi hujaijua na na kuiishi.

Hatua ya kuchukua leo; jua misingi ya asili ni sheria ya usababishi na kisha iishi misingi hiyo na maisha yako yatakuwa mazuri sana.

Kumbuka, maisha ni magumu lakini ni magumu zaidi kwa mpumbavu. Usiwe mpumbavu, pambana, kwani kila kitu kinawezekana.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: