Kuishi kwake Yesu, wakristu wamepona.
Kuishi kwake Mtume Mohammed waislamu wamepona.
Tunaweza kuwa na orodha ndefu ya watu ambao waliishi na kupitia wao na sisi tumepona.
Je, kuishi kwako wewe, watu wanapona?
Unatakiwa maisha yako yawe msaada kwa wengine, kupitia maisha yako na yale unayofanya yanakuwa yanawaponya watu.
Kufungua kwako biashara, wengine watapona. Kuendelea kukaa na ndoto kubwa bila kuifanyia kazi ni hasara kwa dunia.
Najua una mawazo mazuri kweli lakini huyafanyii kazi, pata picha unavyowaua watu wengine kwa sababu wewe hutaki kutumia mawazo uliyonayo na kuyaweka katika vitendo.
Pata picha kama Steve Jobs asingetengeneza kompyuta leo hii dunia ingekuwaje? Ona kuishi kwake Steve Jobs sisi tumepona.
Kufungua kwako biashara watu watapona kwa kuwaajiri, kuwa kwako Bilionea watu wengi watapona.
Kuandika kwako kitabu, watu wamepona. Watu wengi wameendelea kupona yale tunayofanya.
Hatua ya kuchukua leo; hakikisha unatimiza ndoto kubwa ulizonazo, hakikisha unafanya kile ambacho ni sahihi na unajua kitakwenda kuwaponesha watu wengi.
Kitu cha mwisho rafiki yangu nikupendaye, nenda kafanye kile unachopaswa kufanya kwa sababu kupitia hicho utakachofanya watu wengine watapona.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog