Wengi wanaishi kwenye ndoa lakini afya yao ya ndoa siyo nzuri.
Hivi nikiuliza vipi afya yako ya ndoa ndani ya miaka 10 au mitano iliyopita utasemaje?
Ndoa ni biashara kama zilivyo biashara nyingine kwa sababu kwenye biashara, ikiwa biashara haina mzunguko mzuri yaani afya yake haiko vizuri ni rahisi kuanguka.
Kuna vitu vidogo vidogo tu ambavyo wanandoa wengi hawafanyiani vinapelekea ndoa zako kukosa afya.
Kitu ambacho wanandoa wengi hawana ni maana ya pamoja.
Kama Wanandoa mnatakiwa kutengeneza maana ya pamoja yaani create shared meaning.
Kama wanandoa mnapaswa kuwa na malengo makubwa ya pamoja.
Lakini cha kushangaza, wanandoa wengi wanaishi maisha ya ubinafsi. Na kinachotokea ubinafsi unakuwa unazitafuna ndoa zao.
Kwenye maisha ya ndoa, ubinafsi ni shetani mbaya sana, msipoacha ubinafsi, basi maisha ya ndoa yataendelea kuwapiga vizuri sana.
Wanandoa mkishakuwa na ndoto moja ya pamoja, kisha mnasaidiana wote kwa pamoja kila mtu anajua lengo lenu kubwa ni nini mtasaidiana kusukumana na kutembea pamoja.
Lakini, kama unataka mafanikio ya ndoa yenu lakini hamjaungana kwa pamoja katika mchakato sahihi wa kukamilisha kile mnachotaka hamwezi kufanikiwa.
Ila mkikaa chini, mkaweka malengo yenu kwa pamoja na mkakubaliana namna ya kuyafikia inakuwa na nguvu sana kwa sababu ule muunganiko wenu wa kiroho unawasaidia kufanikiwa kwa pamoja.
Hatua ya kuchukua leo; Tengeneza maana ya pamoja na mwenza wako kwenye kile mnachokitaka na kisha tembeeni pamoja.
Kwahiyo, maisha ya uaminifu kwenye ndoa, yanapelekea wanandoa wengi kufanikiwa kwa pamoja.
Lakini, ukiona ndoa haina umoja jua kabisa hapo kuna shida ndoa yoyote ambayo haina umoja kuanguka ni wakati wowote ule. Kama huna umoja na mwenza wako huwezi kutengeneza maana ya pamoja.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog