Pata picha wewe ni meneja wa mauzo na unaambiwa onesha namba ya mauzo ya biashara yako halafu unaanza kutoa maelezo ambayo hayana ushahidi huo unakuwa ni umbea.
Kama wewe ni meneja wa mauzo, au unafanya biashara au kitu chochote kile tuoneshe ushahidi unafanya. Kama huna ushahidi huo unakuwa ni umbea tu.
Ukitaka watu wakuamini kwenye maisha yako ongea kwa ushahidi. Unasema biashara yako inakua onesha namba. Umefanya kitu fulani unataka mtu mwingine akuamini onesha ushahidi.
Uko msemo ambao wanautumia Marekani kwamba tuna tunamwamini Mungu lakini kwa binadamu tunaamini ushahidi.
Hatua ya kuchukua leo; watu wanataka ushahidi, ukisema unafanya kitu au umefanya onesha ushahidi juu ya kitu hicho.
Kama huna ushahidi kwenye kitu chochote kile ambacho unaweza kuonesha jua huo ni umbea tu. Kama huna ushahidi kwenye kile unachosema jua huo ni umbea.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog