Kwa haya yote unayojifunza, kwamba unaweza kupata chochote unachotaka, mawazo yako yanavuta chochote unachofikiria, unaweza kuhisi ni uongo kwa sababu labda wewe umejaribu lakini hujapata ulichokuwa unataka.
Kwa sababu kuna wengine wanapenda kuona matokeo ya haraka, hivyo wakijaribu na kuona hakuna kitu wanaacha kabisa na kukimbilia fursa nyingine.
Kama hivi ndivyo unavyofikiria, basi kuna vitu viwili vinakuzuia usipate kile unachotaka;
Moja; hujakomaa na kitu hicho kwa muda mrefu kiasi cha kuweza kupata unachotaka, huenda unakata tamaa haraka. Pamoja na kwamba inawezekana, haimaanishi utakipata kwa muda unaotaka wewe, upo muda unaopaswa kuwekeza ili kupata chochote unachotaka, na unaweza kuwa muda mrefu sana.
Mbili; hujiamini kama unaweza kupata unachotaka, na hiyo ikapelekea hata usijaribu kabisa.
Au umechukua hatua lakini umeweka nusu nusu, ukijaribu kama labda itatokea, hujaweka juhudi zako zote ukiamini kweli utapata.
Hatua ya kuchukua leo; Fanyia kazi mambo hayo mawili na utaweza kupata chochote unachotaka.
Kitu cha mwisho, kaa kwenye mchakato sahihi kwa sababu maisha ni mchakato na huwezi kupata kile unachotaka kwa muda unaotaka wewe, fanya kazi yako na dunia itafanya kazi yake.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog