Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kupata Fedha Zaidi, Unahitaji Hivi

Kupata fedha zaidi unahitaji kuwa mkubwa zaidi na siyo bora zaidi.

Mtu ambaye kipato chake ni milioni moja kwa mwezi na mtu ambaye kipato chake ni milioni kumi kwa mwezi, unafikiri nani mwenye matatizo zaidi?

Kwa haraka au akili ya kawaida utasema ni mwenye kipato cha milioni moja, kwa sababu ni kidogo ukilinganisha na milioni kumi.

Lakini ukweli ni kwamba, ambaye kipato chake ni milioni kumi ana matatizo zaidi ya yule ambaye kipato chake ni milioni moja.

Kadiri kipato chako kinavyokuwa kikubwa, ndivyo kazi au biashara unayofanya inavyozidi kuwa ngumu, ndivyo changamoto zinavyokuwa kubwa na pia ndivyo hatari ya kushindwa inavyozidi kuwa kubwa.

Hatua ya kuchukua leo;
Kama unataka kuongeza kipato chako, anza kuwa mkubwa wewe kwanza, anza kutatua matatizo makubwa, anza kuwa tayari kukutana na changamoto kubwa.

Kama haupo tayari kwa hayo, hutaweza kuongeza kipato chako. Na msisitizo zaidi muhimu ni ukubwa wa wewe kuweza kupambana na changamoto, na siyo ubora wa wewe kupambana na changamoto hizo.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: