Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ukiwa Na Utulivu Wa Akili

Utaweza kufanya makubwa na kutatua changamoto nyingi zinazojitokeza kwako.

Hata ukiletewa changamoto ambayo wengine wanaona ngumu wewe unaitatua vizuri sana kwa sababu tu umekuwa na utulivu wa akili.

Unapokuwa na utulivu wa akili maana yake uwezo wako wa kufikiri unakuwa juu. Hivyo hata maamuzi unayofanya yanakuwa sahihi kwa sababu hayaongozwi na hisia.

Mtu mwenye hisia anakuwa amevurugwa kiakili na akipata changamoto anakuwa anaitatua kwa hisia ndiyo maana anakuwa anasababisha matatizo zaidi.

Ili uwe na utulivu wa akili, unatakiwa kupata usingizi wa kutosha. Watu wengi ambao wanakuwa hawajapata usingizi wa kutosha wanakuwa hawako vizuri katika utulivu wa akili. Kwa sababu kukosa usingizi wa kutosha inapelekea mtu kupata ulevi fulani.

Kila mtu anajua muda wake wa kulala na kuamka yaani ni masaa mangapi akilala usingizi wake unaisha na anakuwa vizuri sana.

Kupata utulivu wa akili, jitahidi kulala mapema na kuamka mapema. Kwa sababu kulala mapema na kuamka inaleta utajiri, hekima na afya.

Hakuna mtu ambaye analala mapema na kuamka mapema akakosa vitu hivi vitatu, afya, hekima na utajiri. Jitahidi kufanyia kazi hilo na utaona matokeo mazuri.

Kwenye siku yako usijihusishe na vitu ambavyo vinakupa msongo wa mawazo. Kuwa bize na vitu vya maana kama vile kazi na jiepushe na makundi hasi ambayo unajua yatavuruga utulivu wako wa akili.

Epuka kuanza siku yako kwa kusikiliza habari, kutembelea mitandao ya kijamii. Anza siku yako kwa kuamka mapema, fanya sala, tahajudi, mazoezi, soma au sikiliza kitabu.

Hatua ya kuchukua leo; Linda utulivu wako na usikubali vitu ambavyo havikusaidii viharibu utulivu wako.

Yeyote aliyejipanga kuharibu utulivu wako wa akili, mpuuzie, muone au mchukulie kama mtoto ambaye hajitambui na endelea na maisha yako.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: