Ukisoma kitabu cha Predictably Irrational, nguvu zilizojificha ambazo zinatengeneza maamuzi yetu. Mwandishi ametushirikisha sababu tatu kwanini Tunathamini zaidi kile tunachomiliki.
Kwanza tunakuwa tunakipenda, ukikaa na kitu kwa muda unakuwa unakipenda na hivyo kukipa thamani zaidi.
Pili, tunaangalia kile tunachopoteza kuliko tunachopata, hivyo mtu anapouza kitu, anaona kama anapoteza kile anachomiliki na kupenda na siyo kupata fedha ambayo anaweza kuitumia kwa mengine.
Tatu, watu hufikiri kila mtu anaweza kuona ile thamani na upekee wa kitu ambao wao wanaona.
Hatua ya kuchukua leo; fanya maamuzi kwa kufikiri na angalia vitu vyote unavyomiliki na vile ambavyo havina uhitaji viuze ili upate fedha ya kufanya mwingine.
Sababu hizi tatu ndiyo zinawafanya watu kurundikana na vitu ambavyo hawavihitaji, lakini hawapo tayari kuviuza kwa bei ndogo.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog