Design a site like this with WordPress.com
Get started

Sababu Moja Inayosababisha Kutokupata Kile Unachotaka

Watu wengi wana ndoto, wanatamani sana wapate kile wanachotaka lakini kuna kitu kimoja kinawakwamisha.

Na kitu hicho ni hawajaamua kupata kile wanachotaka.

Sikufichi rafiki yangu, kama hujaamua kupata kile unachotaka, huwezi kupata.

Hatua ya kwanza ya kufanikiwa ni kuamua kupata kile unachotaka. Amua kufanikiwa, kama hujaamua kufanikiwa huwezi kufanikiwa kwenye maisha yako.

Watu ambao wameamua kujitoa kweli, dunia imewapa kile wanachotaka kwenye maisha yao.

Kama hujaamua kupata chochote kile unachotaka, kutoka ndani kabisa ya moyo wako, kitu hiko huwezi kukipata.

Kama hujaamua kuwa tajiri, huwezi kuwa tajiri. Utakua na ndoto, utajifunza mengi lakini kama hujaamua kuchukua hatua na kuwa vile unavyotaka wewe huwezi kupiga hatua.

Mafanikio siyo kulazimishwa ila ni hali ambayo inatoka ndani yako kabisa, yaani wewe ukiamua HAKUNA kitachoweza kukusimamisha.

Hatua ya kuchukua leo; Kama bado hujapata kile unachotaka, amua kupata kile unachotaka.

Weka juhudi zinazoendana na kile unachotaka mpaka upate matokeo. Mtu aliyeamua huwa hakwamishwi na kitu chochote kile, vikwazo vyote atakavyokutana navyo atavipangua bila wasiwasi.

Kuamua ni kusema ndiyo mpaka upate matokeo. Mtu aliyeamua kweli kupata kile anachotaka atajituma kweli mpaka afanikiwe kukipata.

Kwahiyo, Sisi binadamu huwa tuna kuwa na nguvu kubwa sana pale tunapoamua kufanya jambo sisi wenyewe bila kulazimishwa hivyo amua kufanikiwa na utafanikiwa kweli.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: