“I do not know where I shall make progress; but I should prefer to lack success rather than to lack faith” Seneca
Ikiwa na maana kwamba, sijui kama nitafanikiwa ,lakini ni bora nikose mafanikio kuliko nikose imani.
Hii sentensi unapaswa kujiambia kila wakati, kwa sababu itakusukuma kutekeleza wajibu wako na kutokukatishwa tamaa na chochote.
Watu wengi wameacha kutekeleza wajibu wao kwa sababu wanakosa imani, wanakata tamaa mapema.
Usikate tamaa, muda utapita hivyo basi, usipochukua hatua unajirudisha nyuma.
Kitu muhimu sana ni kuweka imani yako kwenye mchakato. Tekeleza wajibu wako na simamia.
Huna haja ya kuangalia nyuma au mbele kuna nini kwani unaweza kukatishwa tamaa. Wewe angalia tu nini unapaswa kufanya.
Rafiki, fikiria ni mara ngapi umekuwa na wazo la kufanya kitu cha tofauti kwenye maisha yako lakini hujafanya? Hufanyi wala kutekeleza kwa sababu unakata tamaa.
Hatua ya kuchukua leo; hupaswi kukosa imani iwe utafanikiwa au hutofanikiwa.
Ni afadhali ukose yote lakini usikubali kukosa imani.
Kitu kikubwa ambacho unapaswa kukifanya ni kutekeleza wajibu wako na kuacha kuwa na imani ya kama utafanikiwa au la hilo halipaswi kukusumbua wewe kaa kwenye mchakato sahihi kwa kutimiza wajibu wako.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog