Kitu kinachowarudisha watu nyuma ni kuishi maisha ya kuiga.
Kama unataka kutoka kwenye changamoto za kifedha ambazo tunazo, tuache kuiga maisha ya wengine.
Chagua kuishi maisha yako mwenyewe, kuwa tayari kuchekwa na kuonekana mshamba au wa chini lakini unajua wapi unaenda.
Kama utakua tayari kuishi tofauti na wengine wanavyoishi sasa , baadaye utaweza kuishi tofauti na wengine wanavyoishi.
Usinunue vitu ambavyo huwezi kuvimudu ili tu uonekane nawe upo, uonekane una uwezo.
Hakuna maisha mabaya kama kuigiza una hela halafu huna hela.
Kwa sasa endelea kujenga misuli yako ya kufikia mafanikio makubwa. Usiingiwe na tamaa ya kuiga maisha ya wengine badala yake tengeneza maisha yako kadiri ya kipato chako.
Usinunue vitu ambavyo huvihitaji ili kuwafurahisha watu wasiojali.
Maisha ya kuigiza una hela yana gharama kubwa, ishi maisha yako halisi na utaweza kuwa na uhuru wa maisha.
Hatua ya kuchukua leo; usiishi maisha ya kuigiza.
Ukiendelea kuishi maisha ya kuigiza, utaendelea kubaki kwenye kikwazo vya umasikini.
Usikubali kuigiza maisha, bali ishi maisha yanayoendana na hali yako ya kifedha.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog